MetaTrader 4 (MT4)

Anza na JustMarkets kwa kupakua
jukwaa la kufanyia biashara la MetaTrader 4 (MT4) moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yetu. Nunua na kuuza jozi za sarafu na vyombo vingine vya kifedha kwa kutumia mikataba ya tofauti za bei (CFDs) inayotegemeka na kwa urahisi.

MetaTrader4 interface

Kuhusu MetaTrader 4

Fanya biashara kwenye jukwaa Maarufu

MetaTrader 4 (MT4) ni jukwaa maarufu la biashara, linalopendwa na wafanyabiashara wa ngazi zote. Vipengele vyake na zana mbalimbali zinazonyumbulika hulifanya kuwa rasilimali muhimu kwa mawakala na wafanyabiashara. Pata maelezo kuhusu nini kinachofanya MT4 kuwa ya kipekee na jinsi inavyoweza kuboresha uzoefu wako wa biashara.

MetaTrader4 platform desktop interface

Kutumia MetaTrader 4

MT4 hutoa vitendea kazi mbalimbali, ikiwemo mifumo ya biashara inayoweza kubadilikabadilika, biashara inayotegemea hesabu za algorithmu na biashara inayofanywa kwa simu, iliyoundwa kwa ajili ya wafanyabiashara wenye viwango vyovyote vya ustadi.

Muunganisho unaofaa kwa mtumiaji

Mwonekano wa MT4 huwaruhusu wafanyabiashara wenye kiwango chochote cha uzoefu kuvinjari kwa ufanisi na kutumia vipengele vyake. Jukwaa hili linasaidia kufikia kwa rahisi vitendea kazi vya biashara, zana za chati, na viashiria vya uchambuzi wa kiufundi.

Zana za Hali ya Juu za Uchambuzi

Wafanyabiashara wanaweza kutumia aina nyingi za chati, vipima wakati, na zaidi ya viashiria 30 vya kiufundi vilivyounganishwa ili kuchambua mwenendo wa soko na kufanya maamuzi sahihi ya kibiashara. Jukwaa hili pia linatumia viashiria mahususi na mifumo ya kiotomatiki ya kufanya biashara (Washauri Wataalamu au WW) kwa uchambuzi wa hali ya juu zaidi na mikakati ya biashara.

Uwezo wa Kufanya Biashara Kiotomatiki

Wafanyabiashara wanaweza kuunda, kujaribu, na kutumia Washauri Wataalamu (Expert Advisors) ili kutekeleza mikakati ya biashara kiotomatiki kulingana na sheria zilizoandaliwa mapema. Kipengele hiki kinawezesha kufanya biashara saa 24 siku 7 za juma bila mfanyabiashara kuingilia kati kihalisi.

Usalama Ulioimarishwa

Tovuti hutumia usimbaji fiche wa 128-bit ili kulinda ubadilishanaji wa data kati ya kituo cha mteja na seva. Uthabiti na kutegemeka kwa MT4 huhakikisha ufikiaji thabiti na usioingiliwa wa masoko kwa wafanyabiashara.

Vitu Unavyoweza Kununua na Kuuza kwenye MT4

Aina ya Rasilimali Maelezo Mifano
Fedha za Kigeni Nunua na kuuza mikataba ya tofauti za bei (CFDs) kwenye jozi zaidi ya 100 za sarafu, kutia ndani jozi za sarafu kuu, jozi za sarafu za kiwango cha chini, au jozi za sarafu zisizouzwa au kununuliwa kwa ukawaida. EURUSD, GBPUSD, USDJPY
Bidhaa Nunua na kuuza mikataba ya tofauti za bei (CFDs) kwenye metali na nishati. Machaguo yanatia ndani dhahabu, fedha, gesi asilia, na mafuta. XAUUSD, XAGUSD, BRENT, XNGUSD
Hisa Pata uzoefu utokanao na uteuzi mkubwa wa mikataba ya tofauti ya bei za hisa kutoka tasnia mbalimbali, kama vile teknolojia na matakwa ya watumiaji. AAPL, META, TSLA
Fahirisi za Hisa Nunua na kuuza mikataba ya tofauti za bei (CFDs) kwenye fahirisi kuu za hisa kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani, Japani, na China. Dow Jones, S&P500, NASDAQ, DAX

Kwa nini ufanye biashara ukiwa na JustMarkets

reliability

Tofauti Ndogo & Isiyobadilika Badilika kati ya bei ya kununua na kuuza

Biashara thabiti yenye tofauti ndogo mno kati ya bei ya kununua na kuuza ikianzia pips 0.0, kuhakikisha uthabiti hata wakati ambapo soko linabadilikabadilika mno.

pace

Kutoa fedha papo hapo

Pata pesa zako haraka unapotaka kuzitoa. Chagua kutoka kwenye njia mbalimbali za malipo na upate idhini ya haraka kwa maombi yako.¹

benefits_why_trade_4

Utekelezaji wa haraka

Katika JustMarkets, dili zako zinafanywa papo hapo. Ndani ya sekunde tu, tunahakikisha kuwa biashara zako zinatekelezwa, na kukupa kasi unayohitaji ili kufanya biashara kwa ufanisi.