Nunua na kuuza sarafu za kidijitali bila Ada ya Riba ya Ubadilishaji
Kwa nini ufanye biashara ya sarafu za kidijitali ukiwa na JustMarkets?
Kuanzia sarafu iliyofungua njia ya Bitcoin hadi sarafu zenye ubunifu za Ethereum na Litecoin, JustMarkets inakupa jukwaa la kufuatilia na kufanya biashara kwa kufuatilia kupanda na kushuka kwa bei za sarafu zinazoongoza katika hali ya soko la zenye ushawishi.
Nyenzo mbalimbali za kupima mabadiliko ya bei ya sarafu za kidijitali
Shirikiana na soko la sarafu za kidijitali linabadilika sikuzote ukiwa JustMarkets. Pata uwezo wa kutumia mielekeo ya fahali na dubu ya sarafu kuu za crypto bila haja ya kumiliki mali halisi.
Biashara ya kubadilisha bila riba
Kila mfanyabiashara katika JustMarkets anaweza kufanya biashara bila riba ya ubadilishaji na hakuna matakwa ya ziada, akiruhusiwa kufanya biashara bila malipo ya ziada.
Uwezo wa kutoa fedha haraka
Pata pesa zako haraka unapotaka kuzitoa. Chagua kutoka kwenye njia mbalimbali za malipo na upate idhini ya haraka kwa maombi yako.
Ulinzi dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi
Fanya biashara bila wasiwasi ukiwa na ulinzi wetu dhidi ya mabadiliko ya bei yenye athari hasi. Inazuia mabadiliko ya bei yenye athari hasi, kwa hivyo biashara zako huanzia na kuishia pale unapotarajia, bila kukosa mabadiliko yoyote madogo ya bei.
Usalama wa uwekezaji
Wekeza katika sarafu za kidijitali zenye Ulinzi wa Salio Chini ya Sifuri. Wakati salio linapofika chini ya sifuri kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya ghafla kwenye soko, salio litawekwa sifuri ili kuwalinda wateja dhidi ya hasara zisizotarajiwa.
Utekelezaji wa oda haraka
Katika JustMarkets, dili zako zinafanywa papo hapo. Ndani ya sekunde tu, tunahakikisha kuwa biashara zako zinatekelezwa, na kukupa kasi unayohitaji ili kufanya biashara kwa ufanisi.
Zana za soko la sarafu za kidijitali
Tofauti ya bei wastani
pips
Kamisheni
kwa kila loti/ndani
Dhamana
hadi 1:3000
Malipo ya usiku mrefu
Pointi
Malipo ya usiku mfupi
Pointi
Kiwango cha kuzuia*
pips
Hali ya soko la sarafu za kidijitali
Ingia katika eneo la ubunifu la sarafu za kidijitali, soko lililojengwa kupitia teknolojia ya blockchain ili kuunda na kubadilishana sarafu za kidijitali. Kufanya biashara ukiwa na JustMarkets kunakupa fursa ya kufuatilia mabadiliko ya bei za sarafu za kidijitali na kuinua wasifu wako wa uwekezaji wa mtandaoni bila haja ya kumiliki mali husika.
Saa za kufanya biashara
Ukiwa na JustMarkets, unaweza kushiriki katika biashara ya sarafu za kidijitali saa 24 siku 7 za juma, isipokuwa katika wakati tuliopanga kwa ajili ya matengenezo ya seva. Tutakujulisha kupitia barua pepe na habari kwenye tovuti yetu.
Jozi zifuatazo za sarafu za kidijitali zina mapumziko ya biashara kila siku kuanzia saa 06:00 usiku hadi saa 06:05 usiku: BTCUSD, BTCEUR, BTCGBP, BCHUSD, ETHUSD, LTCUSD, XRPUSD.
| Zana | Kufungua | Kufunga |
| BTCXAU | Jumatatu 01:02 Jumanne – Ijumaa 01:01 |
Jumatatu – Ijumaa 23:57 |
| BTCGBP | 24/7 Mapumziko ya Jumamosi 12:55 – 14:05 |
– |
Muda wote uko katika wakati wa seva (GMT+2).
Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza
Tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza katika soko la sarafu za kidijitali mara nyingi hubadilikabadilika. Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zilizotajwa hapo juu ni wastani uliopatikana kutoka katika biashara za siku za awali. Angalia tovuti yetu ili kuona tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza kwa sasa.
Tofauti kati ya bei za kununua na kuuza zinaweza kuongezeka wakati wa ukwasi mdogo au mabadiliko makubwa katika soko. Hii inajumuisha nyakati kama vile wakati wa mgeuko wa soko, habari mpya kuhusu soko, na matoleo mapya na inaweza kuendelea hadi hali ya kawaida katika soko itakapoanza tena.
Tofauti zetu bora kati ya bei ya kununua na kuuza ni hakika kwenye akaunti yetu ya Raw Spread, ambapo tofauti kati ya bei ya kununua na kuuza huanzia pips 0.0.
Biashara ya kubadilisha bila riba
Riba ya ubadilishaji ni ada inayotozwa kwenye nafasi za biashara za fedha za kigeni ambazo zinabaki wazi usiku kucha. Riba ya ubadilishaji hutofautiana katika jozi tofauti za sarafu. Riba za ubadilishaji hutozwa saa 4:00 usiku GMT+2 kila siku, bila kujumuisha wikendi, hadi nafasi itakapokuwa imefungwa. Ni muhimu kutambua kwamba kwa biashara yenye jozi za fedha za kigeni, riba za ubadilishaji kwa siku ya Jumatano huongezeka mara tatu ili kugharimia gharama za riba za wikendi.
Hutatozwa kwa fahirisi za hisa zilizowekewa alama ya “Waliokubaliwa Ubadilishaji bila riba wanaruhusiwa” katika jedwali hapo juu ikiwa una hali ya ubadilishaji bila riba.
Akaunti zote za wateja kutoka nchi yoyote hupewa moja kwa moja hali ya ubadilishaji bila riba.
Kiwango cha kusitisha
Kiwango cha amri ya kusimamisha biashara ndio umbali wa chini zaidi unaokubalika kati ya bei unayotaka kufungua nafasi nayo na bei ya sasa ya soko wakati unapoweka oda inayosubiri (kama vile Zuia Hasara, Chukua Faida, Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ipande/ Kuuza kwa amri ya kusubiri bei ishuke, au Kipimo cha kunua kwa bei ya chini/ Kipimo cha kuuza kwa bei ya juu). Kiwango hiki husaidia kupunguza hatari ya mabadiliko ya ghafla ya bei (mtelezo wa bei) wakati wa kipindi cha mabadiliko makubwa ya soko, na huhakikisha utekelezaji wa uhakika zaidi wa oda zinazosubiri.
Zingatia kwamba kiasi katika kiwango cha kusitisha kilichoonyeshwa kwenye jedwali hapo juu kinaweza kubadilika na huenda kisiweze kutumiwa na wafanyabiashara wanaotumia mikakati mahususi ya kuchakata oda nyingi haraka au kutumia Washauri Wataalamu.
Matakwa ya kiasi cha dhamana kisichobadilika
Matakwa ya kiasi cha dhamana kwa jozi zote za sarafu za kidijitali hayabadiliki, bila kujali kiwango cha kujiinua kilichowekwa kwenye akaunti yako ya biashara.
Kiwango cha kujiinua
Uwiano wa matumizi ya mtaji kwa sarafu za kidijitali umewekwa kuwa 1:20, lakini unatofautiana kwa baadhi ya jozi.
Sarafu za kidijitali zifuatazo ni zisizo na kufuata kanuni hiyo na zina uwiano ufuatao wa kudumu wa mtaji:
| Vyombo vya biashara | Kiwango cha juu cha kujiinua |
| BTCUSD, BTCEUR, BTCGBP, BTCJPY, ETHUSD, BTCXAU | 1:500 |
| BCHUSD, LTCUSD, XRPUSD | 1:200 |
Programu ya simu ya JustMarkets
Tambua fursa, fanya biashara na udhibiti akaunti zako za biashara ukitumia programu ya JustMarkets Trade. Furahia urahisi wa kuwekana kutoa pesa, machaguo mengi ya njia za malipo na usaidizi wa ndani ya programu kwa saa 24 siku 7 za juma.
Tumia skana kupakua programu
iOS na Android
Maswali yanayoulizwa mara nyingi
1
Sarafu za kidijitali ni nini?
Sarafu za kidijitali, yaani, “crypto” au “cryptocurrency” katika Kiingereza, zinarejelea sarafu za kidijitali au za mtandaoni zinazotumia njia iitwayo cryptography kwa ajili ya usalama. Zinafanya kazi kwenye mitandao yenye usimamizi zaidi ya mmoja kwa kutegemea teknolojia ya blockchain. Sarafu za kidijitali hazidhibitiwi na mamlaka ya serikali yoyote, na kinadharia hilo huzifanya ziwe na kinga dhidi ya kuingiliwa au kuathiriwa na serikali.
2
Teknolojia ya blockchain ni nini, na inafanyaje kazi?
Teknolojia ya blockchain ni daftari kubwa la mtandaoni lisilo na usimamizi wa mamlaka kuu ambalo linarekodi miamala yote inayofanyika katika mtandao wa kompyuta. Inahakikisha usalama na uwazi kwani kila muamala unaongezwa kama kipande kipya kwenye mnyororo na hauwezi kubadilishwa. Teknolojia hii inasimamia sarafu za kidijitali, ikiruhusu miamala salama na isiyojulikana bila kuhitaji mamlaka kuu.
3
Bitcoin ni nini?
Bitcoin, iliyoundwa na mtu asiyejulikana aliyetumia jina bandia la Satoshi Nakamoto mnamo 2009, ni sarafu ya kwanza ya kidijitali na inayojulikana zaidi. Ni sarafu ya kidijitali isiyosimamiwa na benki yoyote ambayo inaruhusu miamala ya mtu kwa mtu bila mamlaka kuu. Miamala ya Bitcoin huthibitishwa na sehemu za kuunganishia mtandao kupitia cryptography na hurekodiwa kwenye daftari kubwa la mtandaoni la umma linaloitwa blockchain.
4
Ni sarafu gani za kidijitali ninazoweza kununua na kuuza?
Kuna sarafu nyingi za kidijitali zinazopatikana kwa ajili ya kununua na kuuza zaidi ya zile zinazojulikana zaidi, Bitcoin na Ethereum. Sarafu hizo ni pamoja na Ripple (XRP), Litecoin (LTC), Cardano (ADA), Polkadot (DOT), na nyinginezo. Upatikanaji wa sarafu hususa za kidijitali kwa ajili ya kununua na kuuza hutofautiana kulingana na jukwaa au mabadilishano unayotumia.
5
Je, ninaweza kufanya biashara ya sarafu za kidijitali kwa kutumia kiwango cha kujiinua?
Ndiyo, majukwaa mengi ya kibiashara hutoa fursa ya kufanya biashara ya sarafu za kidijitali kwa kutumia kiwango cha kujiinua. Kiwango cha kujiinua hukuruhusu kufanya biashara ya kiasi kikubwa kuliko mtaji wako wa sasa, na unaweza kuongeza faida yako. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba ingawa kiwango cha kujiinua kinaweza kukuongezea faida, pia huongeza hatari ya hasara kubwa.
6
Je, ninaweza kufanya biashara wakati wa wikendi?
Ndiyo, tofauti na masoko ya hisa ya kizamani, masoko ya sarafu za kidijitali hufanya kazi saa 24 siku 7 za juma, hii ikiruhusu kufanya biashara mwishoni mwa juma. Hili ni kwa sababu sarafu za kidijitali hazisimamiwi na mamlaka kuu na hazihusianishwi na eneo lolote la kijiografia au chombo kikuu cha udhibiti.